Vigezo Na Masharti

  • 8% itatozwa kwa kila bidhaa itakayouzwa kupitia mfumo kama malipo ya matumizi ya mfumo
  • Wauzaji wanapaswa kuongeza upya bidhaa zilizoisha. Bidhaa hizi hazitaonekana kwa wateja hadi zirejeshwe sokoni.
  • Oda zote lazima ziwasilishwe kwenye ofisi ya usafirishaji ndani ya masaa 24. Zisipowasilishwa, mfumo utafuta oda iyo na kumrejeshea mteja fedha.
  • Malipo ya muuzaji hutolewa kwa sehemu mbili: nusu ya kwanza wakati ofisi ya usafirishaji inapopokea bidhaa, na nusu iliyobaki baada ya masaa 24 tangu bidhaa ifike kituo cha uchukuaji.
  • Mteja anaweza kuanzisha mgogoro ndani ya masaa 24 baada ya kutaarifiwa kuwa bidhaa imefika kituo cha uchukuaji.
    • Mgogoro ukianzishwa, atakayebainika kusababisha atalipia gharama za usafirishaji. Ikiwa muuzaji ndiye mwenye makosa, Tuvae itakata gharama kutoka kwenye malipo yaliyobaki. Malipo hayo yatalipwa tu baada ya mgogoro kutatuliwa.
  • Migogoro mingi hupunguza uaminifu wa muuzaji. Epuka migogoro kadri iwezekanavyo.