Sera ya Kurudisha na Kurejeshewa Fedha/Bidhaa

  • Pindi mteja anapowasilisha oda, muuzaji anatakiwa kushughulikia oda na kuwasilisha bidhaa kwenye ofisi ya usafirishaji ndani ya masaa 24.
  • Iwapo masaa 24 yatapita na ofisi ya usafirishaji haijapokea oda, mteja atarejeshewa fedha kupitia namba ya simu aliyosajili nayo.
  • Ikiwa hali ya bidhaa iliyomfikia mteja ni tofauti na ile ilivyopokelewa na ofisi ya usafirishaji, bidhaa hiyo itarudishwa kwa gharama za ofisi ya usafirishaji.
  • Ikiwa tatizo litatokea, mteja anaruhusiwa kuwasilisha ujumbe wa malalamiko kupitia app ndani ya masaa 24 tangu bidhaa ipokelewe kwenye kituo cha uchukuaji.
  • Yule atakayebainika kusababisha tatizo atawajibika kulipia gharama za usafirishaji za kurudisha bidhaa.
  • Hatua hizi zinaweza kurudiwa mpaka tatizo litakapopatiwa ufumbuzi kamili.